
Barcelona;s 24-year old Argentina striker aliwashinda mchezaji mwenzie wa Barcelona Xavi na mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo katika tuzo hiyo ya mchezaji bora wa mwaka.

Messi, man of the match katika champions league final mwaka 2011, pia alishinda kombe la La Liga, Spanish Supercopa, UEFA Super Cup na Kombe la klabu bingwa ya dunia mwaka uliopita.
Manager wa Manchester United Sir Alex Ferguson na Xavi wote walitoa maneno ya heshima kwa Messi.
Ferguson alisema Messi anaweza kuwekwa katika mizani ya magwiji wa soka duniani katika miaka mingi ijayo, hata kama bado ana miaka 24.
‘Maneno yamekuwa yakisemwa kila kuhusu kwamba wachezaji kama Pele kutoka katika zama za miaka ya 50 wangeweza kucheza katika kipindi hiki, jibu ni kwamba wachezaji wakubwa wanaweza kucheza katika kizazi chochote. Lionel Messi angeweza kucheza katika miaka ya 1950s na sasa pia, kama ilivyo kwa Di Stefano, Pele, Maradona, Cruyff kwa sababu wote ni wachezaji magwiji.” –Fergie

Xavi nae alimuunga mkono Ferguson kwa kusema:” Lionel bado mdogo, ana miaka 24 tu na nafikiri atavunja rekodi zote zilizopo katika huu mchezo. Atakuja kuwa moja ya wachezaji wakubwa waliowahi kutokea katika mchezo huu wa mpira wa miguu.”
Mapema jioni ya jana Ferguson na Pep Guardiola walizawadia tuzo katika shrehe hizo.

Ferguson alizawadiwa FIFA Presidential award for services to football, na alikabidhiwa tuzo hiyo na raisi wa FIFA Sepp Blatter.

Pep Guardiola alitajwa kama kocha bora wa Dunia in 2011 baaada ya kuiongoza Barcelona kushinda makombe matano

Neymar alishinda tuzo ya Puskas kwa kufunga bao bora la mwaka.
Pia jana kilitangazwa kikosi bora cha mwaka kwa mujibu wa FIFA huku kikosi hicho kikitaliwa na wachezaji wa Barcelona, Manchester United na Real Madrid pekee.

KIKOSI CHA FIFA CHA MWAKA
Iker Casillas (Real Madrid), Dani Alves (Barcelona), Gerard Pique (Barcelona), Sergio Ramos (Real Madrid), Nemanja Vidic (Man Utd), Andres Iniesta (Barcelona), Xabi Alonso (Real Madrid), Xavi (Barcelona), Lionel Messi (Barcelona), Cristiano Ronaldo
No comments:
Post a Comment